Jeremiah 4:23-28


23 aNiliitazama dunia,
nayo haikuwa na umbo tena ni tupu;
niliziangalia mbingu,
mianga ilikuwa imetoweka.

24 bNiliitazama milima, nayo ilikuwa ikitetemeka,
vilima vyote vilikuwa vikiyumbayumba.

25 cNilitazama, wala watu hawakuwepo;
kila ndege wa angani alikuwa ameruka zake.

26 Nilitazama, hata nchi iliyokuwa imestawi vizuri imekuwa jangwa,
miji yake yote ilikuwa magofu
mbele za Bwana,
mbele ya hasira yake kali.

27 dHivi ndivyo Bwana asemavyo:
“Nchi yote itaharibiwa,
ingawa sitaiangamiza kabisa.

28 eKwa hiyo dunia itaomboleza
na mbingu zilizo juu zitakuwa giza,
kwa sababu nimesema nami sitarudi nyuma,
nimeamua na wala sitageuka.”

Copyright information for SwhKC